Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga njooni kwa Mkapa ila mtunze akiba ya maneno - Manara

Manara XGSM Day Yanga njooni kwa Mkapa ila mtunze akiba ya maneno - Manara

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kwenda uwanjani na kuujaza uwanja huo kwenye mchezo wa dabi utaaopigwa Jumamosi Aprili 20, dhidi ya watani zao Simba SC.

Manara ambaye amewahi kufanya kazi kama hiyo akiwa Simba amesema pia kuwa, licha ya timu yao kuwa mchezo wa dabi ya Kariakoo ni mgumu kutokana na historia yake, hivyo mashabiki wasiende na matokeo yao mfukoni.

“Mashabiki niwaombe waende uwanjani kwa sababu sisi ni wenyeji. Hii mechi mgao wa hela ni wa kwetu sisi, na klabu zina matatizo chungu nzima, zina majukumu chungu nzima.

“Watu wa yanga tuna tabia moja, mechi kama hii sisi wenyeji badala ya kujaa mnawasumbua vijana waanze kutembea na maspika barabarani ya kazi gani? Nnajua tupo katika ubora wetu, mnajua timu inafanya vizuri, hivi inahitaji spika iende Manzese ‘njooni, njooni… kweli?

“Mtu yeyote mwenye akili lazima uweke akiba ya maneno kwenye dabi kama hii ya Kariakoo. Yanga haendi kucheza na Manyota FC, anaenda kucheza na mkubwa mwenzake. Usipoweka akiba hii unawapa nafasi ya kuzodoa iwapo mechi ikiisha tofauti,” amesema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live