Klabu ya Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya pili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga ASA FC ya Djibouti kwa jumla ya bao 7-0 na sasa Wananchi watakutana kwenye hatua ya pili na Klabu ya Al-Merreikh ya Sudan.
Yanga ina kumbukumbu ya kutolewa kwenye michuano hiyo na Al-Hilal ya Sudan, msimu uliopita na kuangukia Kombe la Shirikisho ambako Yanga ilifanya makubwa mpaka kutinga fainali ya michuano hiyo.
Kwa heshima hiyo, Yanga ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri mbele ya Merreikh kwani wametoka kuwa na msimu bora na bado wana ile hali ya kujiamini.
Yanga wanapaswa kuwaheshimu Al Merreikh kwa sababu ya historia yao, wasifu wao timu ambayo ukija Uwanja wa kimataifa hakuna timu ya Tanzania inayogusa kwenye wasifu bora.
Merreikh wana uzoefu mkubwa na CAF miaka mingi wamekua wawakilishi bora wa CECAFA kwenye CAF Hata kubeba ubingwa wa CAF Ni timu inayopendwa sana Sudan.
Wana mashabiki wafia timu ambao wakati huo hakuna mazuri ya mashabiki ilikua ngumu kupata alama Omdurman, mashabiki wao wana tabia za Mashabiki wa UNAF. vurugu sana.
Miaka kadhaa sasa wanakosa nguvu waliokua nayo kwa mashabiki, na kuyumba kiuchumi, hali iliyopelekea kuomba msaada kutoka kwa matajiri mbalimbali.
Msimu uliopita wa CAF, Merreikh walikua makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika, sambamba na Esperance, CR Belouizdad na Zamalek ambao walimaliza nafasi ya mwisho ikiwa na alama 5, mabao matano ya kugunga na mabao saba ya kufungwa.
Merreikh na kikosi bora, chenye nyota wengi kutoka Latin America hususan Brazil, Hapo walikua na nguvu ya tajiri Ahmed Tata El Tazi raia wa Saudi Arabia ambaye aliondoka mwaka huu mwanzoni.
Kuondoka kwa El Tazi, na hali ya kisiasa Sudan ilipelekea nyota wengi wa kigeni kukimbia, nguvu imebakia kwa wazawa ambao nao sio kama hawatoshi, hapana.
hatua za wali walikuwa wakitumia Uwanja wa Huye uliopo Rwanda kama Uwanja wao wa nyumbani, lakini baada ya kukutana na Yanga wamehamishia Morocco.
Kituo kinachofuata ni Young Africans SC, Yanga wapo kwenye form bora mno, makali waliyokua nayo msimu jana yameendelea msimu huu. Sio wageni tena CAF wanatosha kufanya jambo kwa aina ya mpinzani huyu mwenye Changamoto nyingi kwenye timu yake.
Nani alijua Yanga itampiga Club Africain kwao, nani alijua Yanga itampiga Monastir, nani alijua Yanga itampiga TP Mazembe nyumbani na ugenini, nani alijua Yanga itampiga Real Bamako, nani alijua Yanga italipa kisasi kwa Rivers tena kwao, nani alijua Yanga itampiga Marumo Gallants nje ndani, nani alijua Yanga itatinga fainali ya CAF? Yote hayo yaliwezekana.
Kikosi ni kile kile, kimeboreshwa kidogo na kinaonekana kuimarika zaidi kuliko cha msimu uliopita. Kwa mizania ya kimchezo, Young Africans SC wanaingia kama favorite na Merreikh kama underdog, ila lolote linaweza kutokea Buddah.