Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ni vita Tanga anga ni vita Tanga

638040aa17a795d5165a2f98297b042a Yanga ni vita Tanga anga ni vita Tanga

Thu, 4 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

VINARA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Yanga leo wanashuka dimbani ugenini kuikabili Coastal Union katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mara ya mwisho kukutana ilikuwa Oktoba mwaka jana katika mzunguko wa kwanza wa ligi, Yanga ikiwa nyumbani na kushinda mabao 3-0. Lakini Coastal Union inapokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani bila kujali yupo katika kiwango gani huwa hakubali kufungwa kiurahisi hupambana kupata matokeo mazuri.

Katika michezo mitatu ya hivi karibuni waliyokutana kwenye uwanja huo, Yanga haijashinda mchezo wowote zaidi ya kutoka sare mbili na kupoteza mmoja. Timu hizo zinakutana zikiwa katika viwango tofauti, Yanga ndio timu pekee haijapoteza mchezo wowote wa ligi ikiongoza kwa pointi 49 katika michezo 21.

Michezo mitano iliyopita imeshinda miwili pekee na kupata sare tatu. Ubovu ulioanza kuonekana katika safu ya ulinzi ulimbadilisha kipa kutoka Metacha Mnata na kuwekwa Farouk Shikalo ambaye katika mchezo uliopita hakuruhusu kufungwa, walishinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na Ken Gold mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA).

Katika safu yao ya ushambuliaji bado inaonekana kuna tatizo hakuna maelewano mazuri licha ya kutengeneza nafasi kila mchezo.

Kwa upande wa Coastal Union, wenyewe wako katika nafasi ya 13 kabla ya michezo ya jana ikiwa na pointi 23. Timu hiyo inaoenaka haiko vizuri, ambapo takwimu za michezo mitano iliyopita imeshinda mmoja, imepata sare mbili na kupoteza miwili.

Huenda kupoteza michezo miwili ya mwisho dhidi ya JKT mabao 2-0 na dhidi ya Dodoma Jiji mabao 2-1 kukawafanya kupambana kwenye uwanja wa nyumbani kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Michezo mingine itakayochezwa ni Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa Biashara United. Baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga huenda ikasahihisha makosa ila inakutana na Biashara ambao wako vizuri msimu huu , mchezo utakuwa wenye ushindani.

Polisi Tanzania itakutana na KMC Ushirika Moshi katika mchezo utakaokuwa wenye ushindani mkubwa hasa baada ya wenyeji hao kushindwa kupata matokeo mazuri katika michezo mitano iliyopita ikitoka kupata sare nne na kupoteza mmoja.

Tanzania Prisons itakutana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga. Ni timu zinazojuana unaweza ukawa mchezo mgumu kwa wote wawili ila mgeni ana kazi kwani mwenyeji wake ni mgumu nyumbani.

Chanzo: www.habarileo.co.tz