Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ni mtelezo tu mbele ya Prisons ASFC

Yanga Yanga Kikosi cha Yanga kitaikaribisha Azam FC katika Uwanja wa Azam Complex

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga leo kinarudi kwenye mechi za nyumbani ikitarajiwa kuwa wenyeji wa Tanzania Prisons katika pambano la Kombe la ASFC, litakalopigwa Uwanja wa Azam Complex, kuanzia saa 1:00 usiku, lakini wakipata ulaini kutoka kwa maafande hao wa Magereza.

Prisons iliyo chini ya kocha Abdallah Mohamed 'Baresi', yenyewe imekiri kwamba haitaki kabisa kuumiza kichwa juu ya michuano hiyo ya ASFC, kwani akili zao zipo zaidi kwenye Ligi Kuu ikiwa katika janga la kushuka daraja, hivyo imepania kuelekeza nguvu huko kuliko mechi hiyo ya leo.

Baresi amesema michuano ya ASFC sio kipaumbele kikubwa kwao na kwamba mkazo wameuelekeza kwenye mechi za ligi ambazo ndio zitakazowabakiza kwa msimu ujao, kwani kwa sasa wanahali mbaya zaidi.

"Sio kama hatutapeleka timu au hatutaenda kushindana, lakini kiujumla kitu kikubwa kwetu na muhimu kinachotangulia ni kushinda mechi zetu za ligi," alisema Baresi aliyeipa Mlandege ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2023 ikiifunga Singida Big Stars katika fainali iliyopigwa Janauri 13.

"Tutakwenda kushindana na Yanga lakini ni katika kuijenga kwa utayari timu yetu kuelekea mechi za ligi, hizi mechi za ligi zina kipaumbeele kikubwa kwetu ili tufikie malengo ya kwanza kubaki kwa msimu ujao," aliongeza Baresi.

Aidha Baresi aliongeza bado wanaendelea kuyarekebisha makosa yao ambayo yamekuwa yakijitokeza kwenye ligi ambapo pia watautumia mchezo dhidi ya Yanga kujiimarisha zaidi.

Alisema bado wana imani ya kushinda mechi zilizosalia ili kujiondoa katika eneo la hatari ya kushuka daraja wakiwa katika nafasi ya 14 katika msimamo wenye timu 16 wamebakiza mechi sita wataanza na Namungo Machi 11.

Mechi za Ligi za Prisons

Namungo v TZ Prisons

TZ Prisons v Ruvu Shooting

Geita Gold v TZ Prisons

Kagera Sugar v TZ Prisons

TZ Prisons v KMC

TZ Prisons v Yanga

Chanzo: www.tanzaniaweb.live