Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ni kufa au kupona mbele ya Al Hilal leo

Fiston Mayele Tetema Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele

Sat, 8 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga leo inaikaribisha Al Hilal majira ya saa 10:00 jioni kwenye mchezo wa Klabu Bingwa dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Yanga imefanya vizuri mechi zake za awali za Kimataifa dhidi ya Zalan, ambapo mechi zote walicheza katika uwanja wa nyumbani Benjamin Mkapa na kushinda zote hivyo kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Ni mechi ambayo Mshambuliaji wa Yanga Fiston Kalala Mayele aliweza kupiga hat-trick. Kesho wataanzia nyumbani dhidi ya timu ya Florent Ibenge huku kocha huyo akiwa mzoefu na ligi ya za Tanzania kwani alishawahi kuja kucheza hapa akiwa na Vita Club.

Kocha huyo amefundisha vilabu mbalimbali na Barani Afrika ni mzoefu amepita kunako RS Berkane, Vita Club, ES Wasquehal na sasa AL hilal.

Yanga wanaenda kwenye michuano hiyo baada ya kukaa kwa muda bila kushiriki michuano hiyo, sasa wameanza vizuri na toka mwaka jana hawajapoteza mchezo wa aina yoyote.

Afisa habari wa timu hiyo Ali Kamwe amesema kuwa timu upo vizuri, wachezaji wote wapo tayari na hawana majeruhi kuelekea mchezo wao wa kesho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live