Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ni kazi kazi, Azam wajiangdae kwa kipigo

Konkoni Sure Boy Yanga ni kazi kazi, Azam wajiangdae kwa kipigo

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga SC, kimeendelea na maandalizi ya kujiandaa kuikabili Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 22, mwaka huu.

Kuhusu hali ya kikosi na mazoezi ya timu hiyo, Meneja wa Kikosi cha Yanga SC, Walter Harrison, amesema kila kitu kinaenda vizuri chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu, Miguel Angel Gamondi.

HALI YA KIKOSI “Kwanza tunapenda kumshukuru Mungu tupo salama kabisa, hali ya kambi ipo vizuri kwa wale wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kuziwakilisha nchi zao kwenye wiki hii ya FIFA ndani ya mwezi wa kumi.

“Kila kitu kinaenda sawa mpaka sasa hivi, kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wachezaji ambao wameenda kuwakilisha mataifa yao kwa maana ya wachezaji saba kwa Tanzania, Burkina Faso mmoja, Uganda mmoja na Mali mtu mmoja, tuna takribani wachezaji kumi wametoka kwenda kuziwakilisha nchi zao.

“Kutokana na idadi hiyo kubwa, Kocha Miguel Angel Gamondi ameamua kuwapa nafasi vijana wa timu ya U-20 kuja kujiunga na sisi, tumepata wachezaji takribani nane ambao wametoka kikosi cha U-20.

“Vijana wameweza kuonesha uwezo mkubwa kitu ambacho kimeweza kumfurahisha kocha na inawezekana kuna baadhi ya vijana wakaweza kupata nafasi ya kuja kufanya mazoezi na timu kubwa kwa ajili ya kuendelea kupata uzoefu.

RATIBA YA MAZOEZI “Ratiba ya mazoezi ipo vizuri, timu imerejea mazoezini baada ya mapumziko ya wikiendi, leo timu imefanya mazoezi ya gym pale Gymkhana na kesho Jumanne mazoezi yataendelea pale AVIC jioni kama kawaida.

“Siku itakayofuata kwa maana ya Jumatano mazoezi yatafanyika tena jioni kabla ya kuingia kambini siku ya Alhamisi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunajiweka kwenye mazingira mazuri ya maandalizi kuelekea mchezo wetu wa tarehe 22 dhidi ya Azam FC.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: