Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ni kama Mamelodi na Mamelodi ni kama Yanga tu!

Yanga Vs Mamelodi Yanga ni kama Mamelodi na Mamelodi ni kama Yanga tu!

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imetangaza kwamba katika jukwaa la mzunguko Uwanja wa Mkapa mashabiki wao wataingia bure katika mchezo dhidi ya Mamelod Sundowns wa CAFCL hatua ya Robo Fainali.

Binafsi nauona uongozi wa Yanga umeamua kufanya hivyo ili kupata mashabiki wengi kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji ili mechi waweze kuimaliza hapa hapa kwa Mkapa.

Ni jambo jema kwa sababu hata Mamelodi Sundowns msimu uliopita wa CAFCL 2022/2023 wakati wanacheza Robo Fainali ya CAFCL dhidi ya Petro Atletico mashabiki wao waliingia bure kutokana umuhimu wa mchezo huo.

Sio hiyo tu, msimu huo huo katika mchezo wa nyumbani wa nusu fainali ya CAFCl, Mamelodi ilitangaza kwenye mechi ya MAMELODI vs WYDAD AC kuwa Mashabiki watakaovaa jezi za Sundowns watapatiwa tiketi bure yaani tiketi itakuwa ni jezi ya njano katika uwanjani wa Loftus Versfeld.

Baada ya Mamelodi kutangaza hivyo hakuna Mwandishi au Media ya Afrika Kusini iliyoripoti kuwa ni aibu kwa timu hiyo kubwa kuweka mechi vs Wydad Ac bure, lengo la Mamelodi lilikuwa ni kupata sapoti ya Mashabiki na sio kwamba hawapendi pesa la hasha! Dhumuni ni Mashabiki zaidi ya Pesa, kwa nyakati zile.

Kila Mwandishi na Media za Afrika Kusini zilielewa hili lakini leo Yanga imetangaza kwenye mechi ya YANGA vs MAMELODI eneo la mzunguko ni bure, waandishi na Media nyingi Tanzania wameripoti kuwa ni aibu kwenye mechi kama hii kuweka bure, wanaitupilia baharini sana Yanga kuweka bure na hapo ni mzunguko tu.

YANGA vs SUNDOWNS, kwenye hii mechi Klabu ya Yanga inaangalia zaidi full sapoti ya Mashabiki ili washinde mipambano yao nothing else! Wengine husema Mamelodi haina Mashabiki wengi ndio maana inaruhusu bure.

Mimi nauliza kwanini mechi zingine wanahitaji pesa na zingine bure? Jibu ni kuwa kuna baadhi ya mechi zinahitaji Mashabiki zaidi ya Pesa na Watu wa Marketing ya Yanga wamelifanyia kazi hili.

Tukubali kutokubaliana kuwa Viongozi wa klabu ya Yanga wanajali sana uwepo wa Mashabiki, na wala sio Aibu kama inavyochuliaa na baadhi ya Waandishi na Media!

Wanahitaji watu wajae, Yanga haifanyi kazi kwa sababu za Watu wa Instagram au Twitter, shida watu wanaiabudu Mamelodi kama ndio watu halafu Yanga ni magogo na kushindwa kugundua ndani ni 11v11 hapo uwezo utaamua.

Ni Yanga kutoka Tanzania, ni National Interest kwenye mechi za kimataifa! Content choice ni muhimu! Theory of ​​Keeping a Good Mind.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live