Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ni darasa kwa la mpira kwa Tanzania - Mchambuzi

Yanga Vs Augusburg Yanga ni darasa kwa la mpira kwa Tanzania

Fri, 19 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka nchini, Farhan Kihamu amesema kuwa Klabu ya Yanga ni darasa ambalo vilabu vingine nchini vinapaswa kuiga kutoka kwao.

“Mahusiano kati ya Yanga na vilabu ndio ambayo yamewapa mualiko Afrika Kusini, mahusiano ya Yanga na mawakala ndio ambayo yanawapa wachezaji bora kila wakati, mahusiano kati ya Yanga na vilabu pia ndio haya unaona wanasajili na hakuna kelele.

“Kwa misimu mitatu Yanga imefanya pre-season yao Avic Town na imewapa makombe ya Ligi, FA na fainali ya Shirikisho [CAFCC] lakini sasa wamesogea Afrika Kusini kwa sababu ya mualiko hii inazidi kuwajenga.

“Yanga ni darasa la mpira wa Tanzania, machaguo ni mawili tu aidha uhamasike au uchukie,” amesema Farhan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live