Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Master Tindwa amesema kuwa baada ya Klabu ya Simba kufanikiwa kuwa timu ya kwanza nchini kucheza michuano mikubwa Barani Afrika ijulikanayo kama African Football League, kinachotakiwa ni mwendelezo wa kufanya vizuri zaidi badala ya kubweteka na mafanikio hayo.
Master Tindwa amesema hayo kuelekea mchezo wa ufunguzi wa AFL kati ya Simba SC dhidi ya Al Ahly utakaopigwa kesho Oktoba 20, 2023 katika Dimba la Mkapa.
"Kinachotakiwa ni Consistency. Leo kashiriki Simba kwenye michuano ya African Football League kesho zitashiriki timu zingine.
"Kusema aliyeanza kaanza tu sio sahihi kwa sababu hata Yanga ilikuwa klabu ya kwanza kuingia hatua ya makundi CAF Champions League kwenye ukanda wa Afrika Mashariki lakini leo nani anaekumbuka hili? Hakuna. Cha msingi ni Consistency ya kufanya vizuri," amesema Master Tindwa.