Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ndiyo timu pekee ya Tanzania inayoweza kumtoa Mamelodi

Yanga Vs Mamelodi Yanga ndiyo timu pekee ya Tanzania inayoweza kumtoa Mamelodi

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka Wasafi FM, George Job amesema kuwa, Klabu ya Yanga ndiyo timu pekee kutoka Tanzania ambayo ina uwezo wa kuwafunga mabingwa AFL 2024 na Mabingwa wa CAFCL mwaka 2016, Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini.

Job amesema hayo wakati akizungumza kuelekea mchezo wa Yanga dhidi ya Mamelodi ambao watamenyana kwenye robo fainali Ligi ya Mabingwa Barani Africa huku Yanga akiwa na rekodi ya kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita.

"Daraja la ubora wa Mamelodi liko juu zaidi kuliko Yanga, lakini ukitazama mara ya mwisho Mamelodi kubwa bingwa ni mwaka 2016, tangu hapo amefika nusu fainali mara mbili tu, mara zote amekuwa akiishia hatua ya robo fainali.

"Kumtoa Mamelodi inawezekana lakini inapaswa kuwa na mpango mkakati zaidi. Ukweli ubora wa Mamelodi kuheshimika kwa kufanya ulinganisho wa vikosi vyote viwili.

"Ubora wa Yanga inaweza kuitoa Mamelodi Sundowns na Yanga hii ndio timu pekee kutoka Tanzania ambayo inaweza kuwatoa Mamelod kutokana na ubora wao," amesema Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live