Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ndiyo Bingwa wa Kihistoria wa Kombe la Muungano

Yanga 2023 24 Yanga ndiyo Bingwa wa Kihistoria wa Kombe la Muungano

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga Sc ndio klabu yenye mataji mengi ya kombe la Muungano wafanikiwa kubeba hilo mara sita ikiwa ndio mara nyingi zaidi kuliko klabu nyingine yeyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Yanga wamekuwa Mabingwa wa Kombe la Muungano mwaka 1983, 1987, 1991, 1996, 1997 na 2000.

Katika kombe hili Yanga wana sifa za pekee, moja ni kwamba wao wametwaa Kombe la Muungano mara nyingi kuliko vilabu vyote vya Jamhuri ya Muungano (mara 6).

Sifa ya pili ni kuwa kati ya hizo mara sita ni mara moja tu yaani mwaka 2000 ndio Yanga alikuwa bingwa wa Muungano akiwa sio bingwa wa bara lakini mara tano Yanga amechukua kotekote (Ubingwa wa Kombe la Muungano na Tanzania Bara).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live