Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ndio basi tena African Super League

Yanga X Petro Yanga ndio basi tena African Super League

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Septemba 2,2023 Shirikisho la soka nchini Angola lilitangaza kuifungia klabu ya Petro Atletico de Luanda kwa muda wa miaka miwili kushiriki shughuli yoyote ya soka kufuatia madai ya rushwa ya upangaji matokeo ndani ya ligi kuu nchini humo.

Inaelezwa kuwa mpaka kufikia Septemba 3,2023 CAF walikuwa hawajapokea barua rasmi kutoka Shirikisho la Angola juu ya shtaka hilo huku hofu kubwa ikiwa ni ushiriki wa klabu hiyo kwenye michuano ya African Football League ambayo itaanza kutimua vumbi oktoba 20,2023.

Timu hiyo ya Angola imepangwa kuanza dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini lakini inaelezwa kuwa endapo CAF itapokea barua rasmi kutoka Angola basi itafanyiwa uchunguzi kabla ya maamuzi kutolewa ya kuwaondoa au laah. Aidha uchunguzi utafanyika kwa haraka kabla ya mashindano kuanza mwezi oktoba 2023.

Endapo Petro wataondolewa basi nafasi ya kuziba nafasi yake itabaki ukanda wa kusini mwa Afrika kwani mashindano hayo hayaruhusu ukanda mmoja kuwa na timu zaidi ya tatu na hairuhusu timu zaidi ya moja kutoka kwenye nchi moja kwa awamu hii ya kwanza ya mashindano.

Hivyo Afrika kaskazini tayari haina nafasi endapo Petro ataondolewa kwani tayari ina timu tatu za Wydad,Al Ahly na Esperance.

Kwa Maana hiyo hata Yanga ambayo imekuwa ikizungumzwa kwa awamu hii hawana mlango wa kuingilia katika Mashindano hayo yenye pesa ndefu Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: