Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga narudi muda wowote watakaponihitaji - Tuisila Kisinda

Tuisila Kisinda 28 Winga wa RS Berkane, Tuisila Kisinda

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya jana kuichapa Simba magoli 2-0 mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Winga wa RS Berkane Tuisila Kisinda ameisifu Simba kuwa ni Timu kubwa na yenye uzoefu katika michuano ya CAF isipokuwa kilichotokea ni sehemu ya mchezo wa soka.

Aidha Kisinda pia hakusita kuizungumzia Yanga ambapo amedai yeye Yanga ni nyumbani na yuko tayari kurudi wakati wowote ule atakapohitajika.

“Yanga ndio nyumbani, naikumbuka Yanga, naipenda Yanga, mimi yanga damu tu, namwambia Boss kama anataka nirudi tuongee fresh narudi,” amesema Kisinda

Tuisila Kisinda alipata kupita katika Klabu ya Yanga Kabla ya kuuzwa msimu uliopita kwenda RS Berkane, atarudi tena akiwa na RS Berkane kukipiga na Simba katika dimba la Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live