Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga na upendo wao wa upepo kwa Fiston Mayele

Mayele Mhd.jpeg Yanga na upendo wao wa upepo kwa Fiston Mayele

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miguu inaweza kubeba baraka au laana inapokanyaga kwenye ardhi yoyote ile, ila miguu ya Fiston Mayele ilibeba baraka na utukufu. Wananchi walisimama na Fiston Mayele hata kama alikosea, baraka ilioje!

Mayele hakuanza jana kutoa kauli tata, ila kwa sababu miguu yake ilibeba utukufu na baraka zisizo na kipimo kwenye mioyo ya kila shabiki wa Yanga ilionekana ni sawa.

kila kitu alichokigusa kilionekana dhahabu hata kauli zake tata zilionekana za maana sana.

Ni ngumu kumtengenisha Mayele na mitandao ya kijamii ni kama Amapiano na South Afrika.

Aliwahi kuisema vibaya Mamelord Sundown eti walimcheleweshea 'viza' yake na kupelekea kuikosa mechi ya CAF champion league dhidi ya Mamelord Sundown, inafikilisha

Kauli yake dhidi ya Azam kuwa wanakamia kila wanapokutana na Yanga ilikuwa kauli isiyo ya kiungwana kama mchezaji Professional, lakini mashabiki wa rangi ya njano walimlaki na kumpongeza wakiamini ni kauli ya kishujaa.

Ni chanzo cha vita ya asili baina ya Fiston mayele dhidi ya Zaka zakazi, binafsi nilimuelewa Zaka zakazi zaidi.

Mashabiki wa njano waliendekeza upendo, lakini leo hii upendo wao wenyewe ndio unawatafuna, ni ule upendo uliopelekea upofu dhidi ya kauli tata za Fiston Mayele na kuzipigia kelele mitandaoni kuwa yupo sawa, leo hii kauli zile zile zimewabadilikia na kuwa chukizo.

Unaikumbuka hadithi ya Mrisho ngasa kwenye ubora wake, aliondoka jangwani lakini kila aliporudi, mashabiki wa njano walizidi kutukuza kipaji chake. Kwa sababu hakuthubutu kuisema Yanga vibaya.

Binafsi sijastaajabu kauli ya Mayele dhidi ya viongozi wa Yanga, Ni muendelezo tu wa matukio ambayo mwanzo tulichagua kuyafumbia macho.

Mara nyingi upendo hugeuka chuki. Upendo wa mashabiki wa njano kwa Fiston Mayele asiufanye uwe upendo wa upepo na upendo kugeuka kuwa chuki dhidi yake

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: