Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga na rekodi ya unbeaten miaka mitatu

Yanga WA0042 Yanga na rekodi ya unbeaten miaka mitatu

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mara ya mwisho Yanga kupoteza mchezo wa nyumbani ilikuwa April 25, 2021 chini ya kocha Nabi, hii ina maana kuwa Yanga wamekaa miaka 3 bila kupoteza mchezo wa nyumbani.

Msimu huu Yanga wameshinda michezo 12 ya nyumbani na wamebakisha mechi tatu pekee.

Michezo hiyo ni dhidi ya Kagera Sugar, Tanzania Prisons na Tabora United kama wakishinda michezo yote basi hii pia itakuwa rekodi ya kushinda mechi zote za nyumbani bila sare wala kupoteza mchezo wowote.

Lakini pia wananchi bado ni wababe kwenye kombe la FA sababu huko nako hawajapoteza mchezo wowote.

Toka mwaka 2021 kule Kigoma kwenye dimba la Lake Tanganyika ambapo walipoteza fainali kwa kufugwa bao 1-0 na watani zao Simba SC goli likifugwa na Thadeo Lwanga baada ya hapo Yanga wamekuwa wakitoa dozi kulingana na mgonjwa wanaekutana nae na msimu huu wapo nusu fainali tayari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live