Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga na hesabu kali kwa CR Belouizdad leo

Yanga Kikosi Mds Yanga na hesabu kali kwa CR Belouizdad leo

Sat, 24 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao la dakika ya 48 la kiungo mshambuliaji Hussein El Shahat limetosha kuipa ushindi pekee wa ugenini mabingwa watetezi Al Ahly wakiichapa Medeama ya Ghana kwa bao 1-0.

Ushindi huo wa Ahly unaweza kupokewa vyema na mashabiki wa Ahly kule jijini Cairo Misri na pia nchini Tanzania kwa mashabiki wa Yanga ambao wanaona unaweza kupunguza mlima wa kupanda kwenye safari yao ya kutaka kufuzu hatua ya robo fainali.

Baada ya ushindi wa Ahly ulioifanya kufikisha alama 9, sasa imebaki mikononi mwa Yanga kushinda nyumbani kesho ili kujiweka eneo zuri la kukaribia kufuzu.

Licha ya ushindi huo, Ahly ililazimika kupambana kiume dhidi ya mashambulizi ya Medeama ambao waliwashambulia zaidi Waarabu hao.

Ushindi huo wa Ahly unakuwa pigo kwa wenyeji Medeama wenye pointi 4 mkiani, lakini bado wanayo nafasi ya kusonga mbele kutegemea matokeo ya wapinzani wao kama Yanga na Belouizdad zitatoka sare kesho na kisha zote kupoteza mechi zao za mwisho dhidi ya Al Ahly na Medeama mtawalia. Hii ina maanisha Al Ahly na Medeama wataenda robo fainali.

Kama Yanga na Belouizdad zitatoka sare leo na kushinda mechi zao za mwisho, timu tatu zitakuwa na pointi 9 kila moja na hivyo zitaangaliwa zenye matokeo bora kati yao zilipokutana.

Yanga itamaliza mechi za hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly ugenini Cairo Machi 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live