Uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa wachezaji wote wako katika hali nzuri na wanatarajia kuanza mazoezi katika kambi iliyopo AVIC Town, Kugamboni.
Timu ya Yanga imetoka kucheza mashindano ya Ngao ya Jamii ilipoteza kwa penalti mchezo wa fainali dhidi ya Simba.
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema, “Wachezaji wote wapo vizuri na wanatarajia kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASAS Djibouti unaotarajiwa kuchezwa Jumapili, Uwanja wa Azam Complex.
“Viingilio vya mchezo wetu wa kwanza, Jumapili dhidi ya ASAS Djibouti kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ni VIP A 30,000, VIP B 20,000 na mzunguko ni 5,000.
“Na kuanzia sasa tiketi zimeshaanza kuuzwa makao Makuu ya Klabu Jangwani na tutatangaza vituo vingine kupitia mitandao yetu ya kijamii kwa kufanya hivyo tunawaomba mashabiki wa Yanga wakamilishe zoezi la kununua tiketi mapema.
“Furaha ya wachezaji ni kuona mashabiki wanakuwepo kushangilia na tunaamini itakuwa hivyo kwenye mchezo wa kimataifa ambao tunaamini utakuwa na ushindani mkubwa,”