Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga na TFF wapewa siku saba, vinginevyo watafungiwa

Yanga Supu 6921 Yanga na TFF wapewa siku saba, vinginevyo watafungiwa

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga SC pamoja na Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF vimepewa siku saba kulipa ada ya mwaka za usajili wa Baraza la Michezo Taifa .

Akitoa taarifa hiyo Wakili Evordy Kyando ambaye ni Kaimu Msajili wa Vyama vya Michezo na Mashirikisho vya Michezo nchini, iwapo hawatalipa kwa wakati basi watatozwa faini asilimi tano na hata kufungiwa vyama na shirikisho yao.

"Ndani ya siku saba nimewahifadhi lakini, niliahidi ifikapo Jumatatu ya wiki ijayo orodha hii itakuwa wazi kwenye mitandao, vilabu hivi including Yanga na vinginevyo.

"Simba hadaiwi Simba amelipa kwa hivyo Yanga na wengineyo leo namtaja huyu kama kaka yao mkubwa kama ilivyo Simba ambaye ni kaka yao mkubwa muwaongoze wadogo zenu walipe hizi ada za mwaka kwa wakati," amesema Wakili Evordy Kyando.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live