Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga na Al Ahly watatainga robo fainali - Mchambuzi

Yanga Gamondi Wachezaji Yanga na Al Ahly watatainga robo fainali - Mchambuzi

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya Soka nchini kutoka Wasafi Media, Hans Raphael Mwombeki amewapa nafasi mabingwa wa Tanzania, Young African Sports Club 'Yanga' kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Kauli hiyo ya Hans inakuja baada ya Yanga kupangwa kwenye kundi moja na Medeama ya Ghana, CR Belouzdad ya Algeria na Al Ahly ya Misri.

"Belouizdad ni bingwa wa Algeria misimu minne mfululizo, Al Ahly ni bingwa mara (43) wa Misri na bingwa mtetezi wa CAF, Yanga ni bingwa wa Tanzania misimu miwili mfululizo na finalist wa Shirikisho. Kabla ya kufika hapa Medeama waliwaondoa Horoya ya Guinea, hili ni kundi la kibabe.

"Belouizdad ni tishio kwenye ligi yao Algeria lakini hawana historia nzuri na CAF Champions league kwa miaka ya hivi karibuni. Medeama ni mpinzani wa kawaida kwa Wananchi, hivyo fomu ya Yanga, quality ya wachezaji wao pamoja na "Pira Joga Bonito", Yanga na Al Ahly watatinga Robo fainali," amesema Mchambuzi Hansrafael Mwombeki.

MD1: CR Belouizdad V Yanga Sc (Novemba 24-25, 2023) - Away

Yanga Sc V Al Ahly (Desemba 1-2, 2023) - Home

Medeama V Yanga Sc (Desemba 8-9, 2023) - Away

Yanga SC V Medeama (Desemba 19, 2023) - Home

Yanga Sc V CR Belouizdad (Februari 23-24, 2023) - Home

Al Ahly V Yanga Sc (Machi 1, 2024) - Away.

TotalEnergies CAF Champions League Group Stage Draw Results:

GROUP A: Mamelodi Sundowns (South Africa), Pyramids FC (Egypt), TP Mazembe (DR Congo), FC Nouadhibou (Mauritania)

GROUP B: Wydad AC (Morocco), Simba SC (Tanzania), Asec Mimosas (Cote d’Ivoire), Jwaneng Galaxy (Botswana)

GROUP C: Esperance (Tunisia), Atletico Petroleos (Angola), Al Hilal (Sudan), Etoile du Sahel (Tunisia)

GROUP D: Al Ahly (Egypt), CR Belouizdad (Algeria), Young Africans (Tanzania), Medeama (Ghana).

COMPETITION MATCH DATES

MD 1 | 24 – 25 November

MD 2 | 01 – 02 December

MD 3 | 08 – 09 December

MD 4 | 19 December

MD 5 | 23 -24 February

MD 6 | 01 – 02 March.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: