Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga mzigoni leo kuwakabili Namungo

Yanga Tizi 135 1024x819 Yanga mzigoni leo kuwakabili Namungo

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo saa 12:00 jioni, timu ya Young Africans SC itashuka dimbani kumenyana na Namungo FC ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Huo ni mchezo wa 17 wa Yanga katika ligi hiyo msimu huu ambapo wataucheza kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi.

Young Africans SC itaingia kwenye mchezo huo ikiwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kukusanya pointi 43 zilizotokana na mechi 16, tofauti na kinara Azam FC ambaye amecheza mechi 20, ni pointi moja.

Rekodi zinaonesha kwamba, katika mechi tatu zilizopita walizocheza dhidi ya Namungo nyumbani kwao, hawajapoteza, wameshinda moja na sare mbili.

Wakati rekodi zikiwa hivyo, ikumbukwe kwamba mchezo wa mzunguko wa kwanza ambao Yanga walikuwa nyumbani, walishinda goli 1-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: