Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga mpo! Mwamuzi Saanya kuchezesha Yanga na Simba SC Uwanja Taifa

98128 Waamuzi+pc Yanga mpo! Mwamuzi Saanya kuchezesha Yanga na Simba SC Uwanja Taifa

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwamuzi kiboko wa Yanga, Martin Saanya amekabidhiwa kuchezesha mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba Jumapili Machi 8, ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga wamekuwa na bahati mbaya na mwamuzi Saanya tangu alipoanza kuchezesha Ligi Kuu Tanzania Bara mara kadhaa wamekuwa wakikwaruzana kutonaka na matukio ya uwanjani.

Mwamuzi Saanya mwaka 2009 alikuwa wa akiba wakati Yanga ilipotoka sare na Simba, lakini mwaka 2013 Simba ilipolala mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa ndiye aliyechezesha.

Hata hivyo, Saanya aliingia kwenye mzozo na Yanga baada ya kutoa penalti kwa Coastal Union kwenye dakika za lala salama na mechi kumalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye msimu wa 2012/13, jambo ambalo liliifanya Yanga kumchukia na kukosa imani naye.

Saanya alifungiwa na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) mwaka mzima kwa kushindwa kumudu mechi hiyo ambayo ilisababisha mashabiki wa Yanga kuharibu mali za Uwanja wa Mkwakwani pamoja na basi la Coastal Union.

Kabla ya mchezo huo, mwamuzi huyo alikuwa akituhumiwa na mashabiki wa Yanga kwamba aliibeba Simba kwenye mechi ya hisani dhidi ya Azam. Simba ilishinda mabao 3-2 huku Azam wakidai kunyimwa penalti mbili za wazi.

Pia Soma

Advertisement
Saanya amewahi kuichezesha mechi ya Simba na Yanga msimu wa 2012/13 kabla ya kufungiwa na matokeo ya mechi  hiyo ilikuwa ni sare ya bao 1-1.

Msimu huu Saanya alitofautiana na kocha wa Yanga, Luc Eymael akidai aliinyima Yanga penalti baada ya Bernard Morrison kufanyiwa madhambi ndani ya 18, wakati vijana hao wa Jangwani walipolazimishwa sare 1-1 na Mbeya City.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemtaja mwamuzi Saanya kuwa ndiye atakayechezesha mechi hiyo huku akiwa na wasaidizi sita tofauti ile idadi ya waamuzi wanne iliyozoeleka katika mechi mbalimbali za soka Ligi Kuu Tanzania Bara.

Saanya anayetokea Morogoro, atasaidiwa msaidizi namba moja Mohamed Mkono (Tanga), msaidzi namba mbili akiwa ni Frank Komba wa Dar es Salaam.

Mwamuzi wa msaidizi Elly Sasii (Dar es Salaam na wengine wawili Abdallah Mwinyimkuu (Singida), Ramadhani Kayoko (Dar es Salaam). Mtathimini waamuzi Sudi Abdi (Arusha) na Kamishna wa mchezo Mohamed Mkweche (Dar es Salaam).

Hiyo itakuwa ni mara ya pili kwa mechi ya soka nchini kuchezeshwa na waamuzi sita ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni katika mchezo wa fainali ya Kombe la Azam Sports Federation, uliofanyika katika Uwanja wa Ilulu mjini Lindi, Juni Mosi 2019.

Katika mchezo huo ambao Azam waliibuka na ushindi wa bao 1-0, refa wa kati alikuwa ni Hance Mabena aliyesaidiwa na  washika kibendera, Mohamed Mkono na Ferdinand Chacha huku wa mezani akiwa ni Abubakar Mturo.

Waamuzi ambao walisimama nyuma ya magoli walikuwa ni Saanya na Florentina Zablon.

Chanzo: mwananchi.co.tz