Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga mpo! Diarra aingia kwenye rada za wazungu

Djigui Diarra Maliii Golikipa wa Yanga, Djigui Diarra

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vilabu Mbalimbali Vya Barani Ulaya vikiwemo Kasimpasa , Zenit Saint Petersburg na Dnipro FC vimeonesha nia ya kuhitaji huduma ya Mlinda mlango Wa Klabu ya Yanga SC, Djigui Diarra katika Dirisha kubwa la Usajili la Msimu Ujao.

Taarifa zinathibitisha kwamba vilabu viwili kati ya vitatu vilivyoonesha nia vimeshawasiliana na Management inayomsimamia Diarra na jibu walilopewa ni kusubiri mpaka mwisho wa msimu.

Diarra ambaye Mkataba wake na Yanga unaisha mwezi Mei ni miongoni mwa magolikipa wachache waliowavutia wengi kwenye michuano ya AFCON 2023 kutokana na uwezo wake wa kudaka pamoja na kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: