Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga mpeni unahodha Aucho

Aucho Mwamnyeto M Yanga mpeni unahodha Aucho

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rejea tukio la kukataliwa bao dhidi ya Mamelodi kisha rudi kwenye mechi dhidi ya Kagera sugar utagundua kuwa Yanga nahodha wake kapoa sana.

Mpaka Gamondi anataka kumchapa mwamuzi kutokana na matukio kadhaa yaliyoonesha waamuzi wanainyonga Yanga.

Kuua shambulizi bila sababu ya msingi, Kukataa goli na mengine mengi. Wakati huo wote nahodha Mwamnyeto yeye alikuwa katulia tulii utadhani hakuna kilichotokea.

Nahodha ni kiongozi wa kwanza uwanjani kuitetea timu sio kuvaa kitambaa tu. Mchezaji ninayemuona kwenye matukio mengi kuitetea timu ya Yanga ni Khalid Aucho.

Mpeni kitambaa Aucho au mchezaji mwingine mwenye uthubutu. Kukaa kimya unapoonewa uwanjani ni kuwaruhusu waamuzi kuendelea kuwaonea, kutetea haki kwa nguvu ni kutengeneza fear factor kwa waamuzi hata katika michezo mingine wawe makini.

Kama ulitazama mechi ya jana Champions league Real Madrid dhidi ya Bayern Munich utagundua bila wachezaji wa Real Madrid kumshinikiza mwamuzi akaangalie (VAR) goli lao la pili lingekataliwa.

Nimeona andiko reefu la Ahmed Ally akisema Gamondi hafai kupewa tuzo ya kocha bora kwa sababu ya tukio hili.

Kama ingekuwa hivyo basi Zidane asingepewa tuzo ya mchezaji bora wa kombe la Dunia 2006 kwa sababu alioneshwa kadi nyekundu siku ya fainali baada ya kumpiga kichwa Marco Materazzi.

Sitetei tukio hili ila limechukuliwa kishabiki, Gamondi anastahili adhabu lakini haiondoi ukweli kuwa alikuwa anatetea timu yake baada ya kunyongwa. Mourinho alishaoneshwa red card mara kadhaa na alitwaa tuzo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live