Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga mmewasikia Ruvu shooting, yaita makocha kwa Mkapa

Ruvu Shooting Fc Kikosi cha Ruvu Shooting

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuonekana kama waliokutana nao wamewashindwa ambao ni Kagera, geita Gold, KMC na Azam FC, Timu ya Ruvu Shooting imeapa kumaliza safari ya Wananchi kuibuka na ushindi wa asilimia 100 katika mechi zao.

Yanga ikijiandaa na mchezo wake dhidi ya Ruvu, Jumanne hii katika dimba la Mkapa, Ruvu shooting wao wamewaita makocha wa vilabu vya Ligi Kuu kuja kujifunza ujuzi wa namna ya kucheza na Yanga na kupata alama tatu.

Ruvu wametoa tahadhari kwa Yanga kuwa lazima "mpapaso" uwahusu, na kwamba walimu wa timu nyingine za Ligi Kuu, waje na kalamu kuweka kumbu kumbu ya mbinu watakazozitumia kuwaadhibu Yanga.

Yanga itawakaribisha Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, na Yanga ndio kinara katika Ligi hiyo akiwa na alama 12, akishuka dimbani michezo minne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live