Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga mmesikia salamu zenu kutoka Prisons?

Jeremiah Kisubi Mshambuliaji wa Prisons, Jeremiah Juma

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Maafande wa Jeshi la Magereza ‘Tanzania Prisons’ Jeremiah Juma ameitumia salamu Young Africans, ambayo kwa sasa ipo safari kuelekea mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa.

Young Africans itakua mgeni wa Maafande hao keshokutwa Jumapili (Desemba 19) katika Uwanja wa Nelson Mandela.

Jeremiah ambaye mpaka sasa ndiye mchezaji pekee aliyefunga Hat Trick kwenye Mshike Mshike wa Ligi kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22 amesema: “Yanga wasitarajie mteremko, tunawasubiri kwa hamu tuliwaona kwenye mechi zao, lakini niwaombe mashabiki waje kwa wingi waone pira gwaride, tutakomaa na kuweka rekodi Jumapili.”

Tanzania Prisons itakwenda kusaka alama tatu muhimu dhidi ya Young Africans, ikiwa nafasi ya 13 katika Msimamo wa Ligi hiyo kwa kufikisha alama 8, huku wageni wao wakiwa kileleni kwa kumiliki alama 20.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live