Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga mdomoni mwa Wa-nigeria CAF

Yanga Sc New Coach Nasreddine Nabi In Session 1lbq2oo3ka73l1oktqvv0oirvh Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi

Sat, 14 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Hatimaye kile kitendawili cha nani atakwenda wapi na nani atacheza na nani rasmi kimeteguliwa baada ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kutoa ratiba ya michuano hiyo msimu huu.

Yanga itaanzia nyumbani dhidi ya Rivers United ya Nigeria katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika katika mchezo utakaofanyika kati ya Septemba 10-12 kabla ya kurudiana wiki moja baadae.

Timu ya Rivers United maskani yake yako kwenye Uwanja wa Yakubu Gowon uliopo katika mji wa Port Harcout nchini Nigeria.

Yanga imepata nafasi ya kushiriki michuano hiyo baada ya kumaliza ya pili katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, kufuatia Tanzania kupata nafasi ya kuwakilishwa na timu mbili katika michuano hiyo pamoja na ile ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba ambayo itaanzia raundi ya kwanza, wenyewe ndio Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na walifikia hatua ya robo fainali msimu uliopita katika michuano hiyo, huku Namungo ikishiriki Kombe la Shirikisho la kucheza hatua ya makundi.

Msimu uliopita, Simba walianza na timu ya Nigeria ya Plateua United na kushinda bao 1-0 na kusonga mbele hatua inayofuata.Lakini safari hii atakaa kusubiri mtu atakaeshinda ili akutane nae.

Mabingwa wa Tanzania Bara Simba, ambao wataanzia raundi ya kwanza, wenyewe watacheza na mshindi kati ya Jwaning Galaxy ya Botswana dhidi ya DFC Arrondissement ya Afrika ya Kati.

Wakati huohuo, Azam FC nao wataanzia nyumbani dhidi ya Horseed ya Somalia, huku Biashara ya Musoma Mara, wenyewe wataanzia kwa kukipiga ugenini dhidi ya AFC Dikhil ya Djibout katika mechi za Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz