Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Fredrick Mwakalebela amewatoa hofu mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kuwa hakuna tatizo kwenye klabu hiyo licha ya kucheza dakika 270 bila ya kufunga goli kwenye michezo mitatu waliyoicheza kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2021/22.
kauli hiyo ameitoa Mwakalebela kuelekea mbio za ubingwa wa ligi kuu baada ya kutoka suluhu dhidi ya maafande wa Magereza klabu ya Tz Prisons kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam
“hakuna tatizo lolote zaidi ya tatizo la kiufundi,sisi plan zetu (A na B) zilishindwa kufaulu na tunapaswa kukubali matokeo maana ndio maana halisi yamchezo wa mpira ,bado tuna mechi nyingi za kutengeneza pengo baina ya yetu na wanaotufatia na bado tupo kwenye mbio za ubingwa”amesema Mwakalebela
Yanga ipo kileleni mwa msimamo wa NBC premier league wakicheza michezo 23 na wakiwa na alama 57 huku Simba ambao ni mabingwa watetezi wakishika nafasi ya pili wakiwa na alama 46 huku kesho wakishuka dimbani kupambana na klanu ya Kagera Sugar siku ya Jumatano ilhali michezo saba imesalia kumalizika kwa ligi hiyo kwa msimu huu.