Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga mbioni kumnasa Ranga Chivaviro

Kaizerrr Hersii Yanga mbioni kumnasa Ranga Chivaviro

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sahau kuhusu Kipigo walichopata Yanga dhidi ya CR Belouizdad jana usiku. Wananchi wameanza mchakato wa kumsainisha mshambuliaji wa Kaizer Chiefs, Ranga Chivaviro.

Awali ilimtaka staa huyo lakini ikashindwana naye dau dakika za mwisho akaenda Kaizer.

Tayari kocha wa Yanga, Gamondi amekaririwa mara kadhaa akisema anahitaji mshambuliaji anayejua kufunga kutokana na Hafiz Konkoni kushindwa kuonyesha kile kilichotarajiwa aliposajiliwa kuziba nafasi ya Fiston Mayele aliyeuzwa Pyramids ya Misri.

Mabosi wa Yanga wameanza utekelezaji huo sambamba na kusaka winga anayetakiwa pia na kocha Gamondi wakivizia dirisha dogo la usajili linalofunguliwa Desemba 16 na kufungwa Januari 15, mwakani.

Yanga inamvizia Chivaviro kwavile analijua goli, lakini hachezi michuano ya CAF, ili iwe rahisi kumtumia kipindi hiki timu hiyo ikicheza makundi ya Ligi ya Mabingwa, ingawa wanaweza kukumbana na bei kubwa ubaoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live