Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kwenda robo fainali CAFCL ni kudanganyana - Jembe Ulaya

Pacome Gamondi Maxi Yanga kwenda robo fainali CAFCL ni kudanganyana - Jembe Ulaya

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' pamoja na vilabu vya Yanga na Simba, Bakari Malima 'Jembe Ulaya' ametoa maoni yake kuhusu mchezo wa marejeano wa Ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi, Yanga SC dhidi ya Medeama FC ya nchini Ghana huku akiwataka mashabiki wa klabu hiyo kumpa muda zaidi kocha Miguel Gamondi kwaajili ya kuiandaa timu na siyo kutoa presha kuelekea mchezo huo.

Jembe Ulaya amesema kuwa, Yanga mpaka sasa wameshafikia malengo yao Kimataifa msimu huu, hivyo wanapaswa waongeze wachezaji wenye ubora zaidi ili kwenda mbele ya hapo walipofikia.

"Wapenzi na Wanachama wa soka wanatakiwa watofautishe kati ya Shirikisho na Ligi ya Mabingwa, kule unakutana na wanaume wa shoka sio shirikisho. Nabi alifanya ya kwake mazuri akaondoka, tunamsifu. Ni kipindi sasa cha kumwachia timu mwalimu Gamondi aitengeneze kwenda kushiriki Klabu Bingwa ikiwa bora zaidi.

"Watu wasifananishe mafanikio ya shirikisho na klabu bingwa, ni tofauti sana. Gamondi aachiwe afanye kazi kwa ufahasa, aletewe wachezaji, kumlaumu sasa hivi ni kumuonea tu. Kwa kikosi hiki cha Yangani kizuri zaidi kwa Ligi ya Tanzania lakini Klabu Bingwa inatakiwa aongezewe watu wa kazi.

"Kuna baadhi ya wachezaji Yanga wameonyesha ni bora kwa mfano Maxi, Pacome, Aziz Ki, sasa inatakiwa waongezwe wachezaji wenye ubora kumzidi Pacome, Maxi na Aziz Ki ili Yanga iende robo fainali, nusu fainali ya CAFCL.

"Lakini tukisema msimu huu Yanga iende robo fainali tutakuwa tunadanganyana na hatuusaidii mpira wetu wa Tanzania," amesema Jembe Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live