Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kwenda na hapa kazi tu

475c453928a8e0a80ab0fb447f287f1e.jpeg Yanga kwenda na hapa kazi tu

Sun, 28 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamesema watakwenda na kauli mbiu ya Rais John Magufuli ya Hapa Kazi tu katika mechi zao zilizobaki ili kutimiza lengo lao.

Hapa Kazi Tu ni kauli mbiu iliyoanzishwa na Magufuli enzi za uhai wake iliyomuongoza kutimiza majukumu yake ya kitaifa.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana Kaimu kocha mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi alisema wamedhamiria kufanya kazi na hilo watalidhihirisha katika mechi zijazo.

“Mwendo tutakaoenda nao ni Hapa Kazi tu, tunataka kufanya kazi kutimiza kile tulichokusudia, ni muhimu kwetu kujipanga na kufanya vizuri,”alisema.

Alisema kikosi chake kinaendelea kujifua kujiweka imara wakati wakisubiri baadhi ya wachezaji wanaotumikia timu zao za taifa kurudi.

Mwambusi alisema hakutakuwa na programu za mechi za kirafiki kwa vile bado kuna maombolezo hivyo watajifua wenyewe huku wakisubiri kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam.

Kocha huyo aliyepata mafanikio katika klabu hiyo akiwa na Hans Pluijm, msimu wa 2015 hadi 2017 alisema anahitaji wachezaji wanaojituma na kujua majukumu yao uwanjani na kwamba anaamini waliopo hawatamuangusha kwani kila mmoja ni muhimu.

Kocha huyo ambaye pia, amewahi kuifundisha Mbeya City amekabidhiwa mikoba ya Cedric Kaze ambaye alitimuliwa kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo.

Lakini Mwambusi alikuwa ni msaidizi wa Kaze kabla ya kuomba kupumzika akidai ni mgonjwa na walipata mafanikio baada ya kuchukua Kombe la Mapinduzi Zanzibar mapema mwaka huu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz