Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuzindua ofisi bora Afrika Mashariki na Kati

Yanga Kuzindua Ofisi Bora Afrika Mashariki Na Kati.jpeg Yanga kuzindua ofisi bora Afrika Mashariki na Kati

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Club ya Yanga SC inatarajia kuzindua ofisi zake katika Makao Makuu ya club hiyo baada ya kufanyiwa ukarabati na maboresho ambapo club hiyo imesema kuwa ofisi hiyo kwa sasa ndio bora zaidi Afrika Mashariki na Kati.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC Ally Kamwe amesema;

“Leo rasmi tumeingia kwenye wiki ya anniversary ya club hii kubwa Tanzania kuelekea kilele cha Birthday ya Young Africans SC tarehe 11 mwezi huu wa pili, safari hii tuna mambo makubwa, hii ni wiki yetu wenyewe, kesho Young Africans SC tutakwenda kusaini mkataba na Hospitali kubwa sana duniani, ikiwa na lengo la kumnufaisha shabiki wetu kwenye masuala yanayohusu afya yao, Klabu kubwa lazima iwaze kwa ukubwa namna gani Mwanachama wake atanufaika na club kubwa”

“Siku ya jumatano, pale makao makuu ya Jangwani, tunakwenda kuzindua upya ofisi zetu, Uongozi umefanya ukarabati wa kihistoria ambao umeifanya Young Africans SC kuwa na ofisi bora zaidi Afrika Mashariki na Kati”

“Tuna mpango wa kutuma mwaliko rasmi kwa vilabu vingine kuja kushuhudia uzinduzi wa kihistoria wa ofisi za Young Africans SC, tunaposema makao makuu ya club kubwa tunamaanisha historia nzima ya club ipo, tumehakikisha tumepata makombe ya zamani ambayo tumewahi kushinda, ni uzinduzi uliobeba dhima ya historia ya club yetu”

“Tarehe 8, tunakwenda kufanya uzinduzi ambao utasimamisha Nchi, tukio hili linakwenda kuonesha mwelekeo wa club hii, ni miongoni mwa mambo ambayo yanafanywa na Madrid na Bayern huko, nawasihi Wachambuzi wajitokeze kwa wingi tunakwenda kumaliza ile kiu yao, tunakwenda kuzindua nyimbo mbili kubwa kwa lengo la kusheherekea kilele cha anniversary ya mabingwa wa kihistoria, yaani kuelekea kwenye hiki kilele ni jiwe juu ya jiwe, hakupoi kila Mwanachama anapaswa kuweka kambi Mbeya.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live