Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuzindua kitabu chao leo

Yanga Yapokea Ofa Ya Wachezaji Watano Yanga kuzindua kitabu chao leo

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo Jumamosi, Juni 15, 2024 ni uzinduzi wa kitabu cha Yanga kwenye Ukumbi wa Hyatt Regency, Kitabu hicho kinachotarajiwa kuzinduliwa na uongozi wa timu hiyo umebainisha kwamba umekusanya mengi ya muhimu bila kuacha chochote.

Ipo wazi kwamba kwa msimu wa 2023/24 Yanga imetwaa taji la Ligi Kuu Bara, CRDB Federation Cup na ilitinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa jambo hilo la uzinduzi wa kitabu limekuwa likisubiriwa kwa shauku kubwa limefanyika kwa umakini mkubwa ili kuwapa yale yaliyo muhimu mashabiki na wanachama.

“Ni jambo la kihistoria tunakwenda kufanya Yanga ni klabu yenye miaka 89 na kuna mengi ambayo wanachama na mashabiki wanahitaji kuyajua kazi hii tumeanza kuifanya miezi saba iliyopita na safari hii hatujaacha chochote.

“Mashabiki na Wanachama wanahitaji kupata kile kilicho bora na tunaamini kupitia hiki kitabu kuna simulizi nyingi nzuri watakutana nazo ambazo zinaeleza namna ilivyokuwa tangu awali mpaka sasa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live