Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuweka kambi Ulaya

Hersi Yanga Gamondiz Yanga kuweka kambi Ulaya

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Yanga umebainisha kuwa mpango mkubwa ni kuweka kambi Ulaya ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2024/25. Yanga ni mabingwa wa ligi msimu wa 2023/24 walitwaa taji hilo baada ya kufikisha pointi 71 na walimaliza msimu wakiwa na pointi 80 kibindoni.

Leo Juni 15 2024 wanatarajia kufanya uzinduzi wa kitabu cha historia ambacho kitakusanya matukio yote muhimu yaliyopita ndani ya miaka 89 ya timu hiyo.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa mpango mkubwa kwa msimu ujao ni kufanya vizuri zaidi na wanatarajia kuweka kambi Ulaya huku kukiwa na mialiko kutoka nchi nyingine ambazo zinahitaji kuona timu hiyo inakwenda kucheza mechi za kirafiki.

“Kuelekea maandalizi ya msimu mpya tunatarajia kwenda Ulaya na kumekuwa na mialiko kutoka nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, Kenya kote huko nah ii inatokana na ukubwa wa timu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live