Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuwafuta Kagera Sugar, Mwanza

314922670 211102737962497 8934788097358010952 N Yanga kuwafuta Kagera Sugar, Mwanza

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: eatv.tv

Kikosi cha Yanga leo Novemba 11 kimerejea Dar Es salaam na kinatarajia kuanza safari kuelekea Mwanza.

Ni safari ya kutoka Tunisia ambayo ilianza jana Novemba 10 na walipitia Dubai kabla ya kuibukia Dar.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kimetoka kupata ushindi wa bao 0-1 dhidi ya Club Africain na kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye msafara huo ni pamoja na Kibwana Shomari, Aboutwalib Mshery, Farid Mussa.

Jumapili wana kazi ya kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema wamefurahi kurejea na ushindi ni zawadi kwa Watanzania.

“Tumerejea salama na ni furaha kwetu kuona tumepata ushindi ni zawadi kwa Watanzania na tuna kazi Mwanza Jumapili mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”

Chanzo: eatv.tv