Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuwafuata Watunisia Kesho

Yanga Kikosi Al Hilal 1140x640 (1) Kikosi cha Yanga

Thu, 3 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msafara wa watu 41 wa Young Africans SC utasafiri kesho saa 9:25 mchana kuelekea Tunisia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain.

Msafara huo wenye wachezaji 22, benchi la ufundi 10 na viongozi 9 utaondoka nchini kwa Shirika la ndege la Emirates na unatarajia kutua Dubai, saa 9:45 usiku.

Baada ya kutua Dubai, msafara huo utalala hapo kisha Novemba 5,2022 kuanza safari saa 2:00 asubuhi kwenda Tunisia na kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Carthage, mjini Tunis majira ya saa 6:35 mchana kwa saa za Tanzania.

Mara baada ya kuwasili Tunis, Yanga wataanza safari kwenda mji wa Sousse, mwendo wa saa 1:30 kwa basi na kuweka kambi huko kwa siku 2.

Novemba 7,2022 jioni, msafara utarejea Tunis, na kupumzika kabla kesho yake kwenda kwenye uwanja wa Hammedi Agrebi Olympic, kwa ajili ya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo.

Mchezo unatarajiwa kupigwa Novemba 9, 2022 majira ya saa 10: 00 jioni kwa saa za Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live