Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuwafata Al Merrikh Septemba 14

Yanga Rekodi Mpyaaaaa.jpeg Kikosi cha Yanga

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Yanga imesema itaanza safari ya kuelekea Rwanda Septemba 14 kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza hatua ya mtoano kufuzu makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga itamenyana na Al Merrikh ya Sudan mchezo utakaopigwa nchini Rwanda katika Uwanja wa Pele Septemba 16.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Ofisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amsesema;

"Timu inatarajia kuondoka tarehe 14.09.2023 (Alhamisi) kuelekea Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kwanza raundi ya pili #CAFCL dhidi ya Al-Merrikh SC.

Najua watanzania wengi wanayo kiu ya kwenda kushuhudia mchezo wetu dhidi ya Al-Merrikh. Klabu imeaanda mpango wa kusafiri na mashabiki kutoka hapa Dar es Salaam kwenda Kigali, Rwanda. Wachezaji na benchi la ufundi watasafiri kwa njia ya anga, mashabiki na Viongozi watasafiri kwa njia ya basi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: