Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuwacheka Simba kuishia robo ni ushamba

MAshabiki Yanga Taifa 1140x640 Yanga kuwacheka Simba kuishia robo ni ushamba

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siwezi kuilinganisha Simba na Yanga kimataifa , Kimataifa Mfano wa Simba ni Simba yenyewe, Yanga hajakutana na team ngumu kimataifa misimu ya hivi karibuni kiasi kwamba tuanze kuifananisha na Simba

Ili tuanze kuifananisha Yanga na Simba kimataifa ni lazima Yanga washinde Match dhidi ya timu kubwa na bora Africa, iongoze kundi CAFCL mbele ya  Al Ahly, Wydad, Orlando Pirates, AS Vita, RS berkane, ASEC Mimosas, Kaizer Chiefs, Raja Casablanca na nyingine.

Msimu uliopita ndipo Yanga angalau ilijipapatua na kufanya vyema kwa kufika fainali ya CAFCC. Njiani walikutana na Zalan, Al Hilal ikawatoa CAFCL na kuangukia CAFCC, wakakutana na Club Africain ambapo walitoboa kwenda makundi.

Huko kwenye makundi wakakutana na TP mazembe iliyochoka, US Monastir na Real Bamako. Robo fainali wakakutana na Rivers United, nusu fainali Marumo Gallants na fainali USM Alger. Unaweza kuona njia yao ilivyokuwa ngumu au nyepesi.

Yanga ina timu nzuri na wachezaj wazuri lakini huku Kimataifa bado hawajafanya makubwa kama ambavyo watazi zao wamefanya kwa miaka sita sasa.

Msimu huu Yanga wapo group stage ya CAFCL na Al Ahly, CR Belouzidad na Medeama. Hapa kidogo Yanga ataanza kuonja ladha ya utamu na uchungu wa group stage za CAFCL baada ya kuikosa kwa miaka 25 akiishia preliminary stages.

Unaweza kuona Simba kuishia Robo Fainali kama Jambo rahisi lakini Group Stage itakapoanza ndipo tutakuja kuipa heshima Simba. Yanga wanapaswa wapambane kikubwa ili kuutafuna mfupa ambao umekuwa ukimshinda Simba kila mwaka na kukomea Robo.

Yanga kuwacheka Simba kuishia robo fainali ya CAFCL ni ushamba, wanachopaswa kufanya ni kutia juhudi na kufanya vizuri zaidi kuliko kumcheka mtu kwa hatua aliyofikia wakati wewe hujawahi hata kuisogelea kwa miaka 25, achana na kuifikia, nazungumzia kuisogelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live