Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuvunja Mkataba na Azam, kususia bidhaa za Azam

Wazee Yanga Di Wazee wa Yanga na Viongozi wa matawi Yanga

Wed, 28 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vita ya chuki ni kama imechukua nafasi hivi baada ya sakata la kiungo wa Yanga Feisal Salum kutaka kuvunja Mkataba na kutimkia Azam FC.

Wakati sakata hilo likiwa bado linaendelea kufukuta wazee wa Yanga na viongozi wa Matawi wamekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia skata hilo.

Kitendo cha Feisal kutaka kuondoka Yanga na kutajwa kujiunga na Azam ni kama kimeibua chuki kwani wametoa azimio zito kuelekea kwa Kampuni ya Azam na bidhaa zake

" Kama Viongozi wa Yanga wakibaini Azam FC ndio wanamdanganya Feisal Salum aende kwao basi tunawaomba Viongozi wetu wavunje ule mkataba wetu na Azam halafu na sisi mashabiki wa Yanga hatutanunua bidhaa zozote za Azam " wamesisitiza wazee hao

Chanzo: www.tanzaniaweb.live