Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kutupa karata yao ya mwisho leo

Africain Club Vs Yanga Yanga kutupa karata yao ya mwisho leo

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: Nipashe

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kufuzu makundi Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga leo inashuka dimbani katika mchezo wa marudiano wa michuano hiyo utakaopigwa Tunisia.

Mchezo huo wa marudiano utafanyika katika uwanja wa Olympique Hamadi Agrebi uliopo eneo la Radès katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam Novemba 2 timu hizo zilitoka suluhu.

Akizungumza na mtandao wa Yanga akiwa Tunis Kocha Msaidizi wa klabu hiyo, Cedric Kaze amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika, wachezaji wote wapo katika hali nzuri na wana matumaini makubwa ya ushindi.

“Ni mchezo wa maamuzi dhamira yetu ni kushinda na maandalizi tuliyoyafanya tukiwa kambini huko Sousse mpaka tumefika hapa Tunis yametupa matumaini kwamba tunaweza kufanya kitu na kuwashangaza watu,” amesema Kaze.

Yanga inalazimika kushinda au kupata sare ya idadi yoyote ya mabao ili kusonga mbele hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Mguu Afrika(CAF).

Chanzo: Nipashe