Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kutua Dar kesho

Yanga Yamshushia Nabi Mvua Ya Magoli 4 0.png Yanga kutua Dar kesho

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Kombe la Toyota 2024, Yanga wanatarajia kutua nchini kesho Julai 30, 2024 wakitokea Afrika Kusini.

Yanga inatua nchini kibabe baada ya kuifunga Kaizer Chiefs jana kwa Mabao 4-0 na kutwaa ubingwa wa Toyota kwa mwaka 2024.

Mabao ya yaliyoipa Yanga ushindi yalifungwa na Prince Dube, Clement Mzize na Stephane Aziz Ki akifunga mawili.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa kocha Nasreddine Nabi akikaribishwa na kichapo hicho kutoka kwa waajiri wake wa zamani.

Kikosi cha Wananchi kinatua Dar kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Mwananchi ambayo kilele chake ni Agosti 4, mwaka huu ikitamatishwa na mechi dhidi ya Red Arrows.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live