Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kutimka leo, Nabi atua Tunisia mapemaa

Yanga Wqed Yanga kutimka leo, Nabi atua Tunisia mapemaa!

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kikosi cha wachezaji 25 cha Yanga kinaondoka leo Februari 7 saa 9:25 alasiri kwenda Tunisia tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika kocha wa kikosi hicho, Nasreddine Nabi tayari yuko nchini humo kuweka maandalizi sawa.

Yanga itaikabili Monastir ya Tunisia Februari 12 kwenye uwanja wa Olympique Hamadi Agrebi uliopo mji wa Tunis.

Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema kikosi hicho kitasafiri bila kocha wake Nasreddine Nabi ambaye alisafiri kwenda Tunisia baada tu ya kumalizika mechi ya ligi dhidi ta Namungo iliyofanyika Jumamosi iliyopita.

"Timu itasafiri kuelekea Dubai tutafika saa 3:50 usiku itapumzika pale usiku wa leo halafu kesho asubuhi saa 2:40 kikosi kitaondoka kutoka Dubai kulekea Tunis kwa ajili mchezo huu.

" Timu itaondoka na wachezaji 25 lakini pia ndani yake yuko kipa Aboutwalib Mshery ambaye yeye haendi Tunisia kama sehemu ya mchezo bali anakwenda kwa ajili ya matibabu kwa sababu anatakiwa kufanyiwa upasuaji," amesema Kamwe.

Kamwe amesema msafara hautakuwa na kocha Nabi ambaye alishatangulia Tunisia muda mrefu na anaisubiri timu huko.

"Pia msafara utakuwa na viongozi tisa akiwemo mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Seif Gulamali na mkuu wa msafara ni Mrisho Bukuku mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)," amesema Kamwe.

Pia Kamwe amesema wakati timu ikiondoka leo tayari wameshaanza maandalizi ya mchezo mwingine wa hatua hiyo dhidi ya TP Mazembe utakaofanyika Februri 19 kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia saa 1:00 jioni.

"Fanya ufanyavyo ila pointi za nyumbani ni muhimu kweli kweli kwenye mahesabu yako na ndio maana timu inasafiri leo kwenda Tunisia kwa ajili ya mchezo dhidi ya Monastir ambao pia ni muhimu lakini nguvu tumeiweka pia katika mchezo ujao wa TP Mazembe.

"Tumeanza maandalizi ya mechi yetu ijayo dhidi ya Mazembe na yanahusisha uuzwaji wa mapema wa tiketi za mchezo huo na wakati leo timu inasafiri pia tiketi za mechi hiyo zimeshaanza kuuzwa, " amesema Kamwe na kuongeza;

"Tiketi zitakuwa VIP A sh 30000, VIP B ni Sh20,000 na VIP C Sh10,000 wakati mzunguko ni Sh 3,000 kuanzia leo lakini siku ya mchezo huo tiketi utaipata kwa Sh 5,000 na yote ni kutaka kujenga utamaduni wamashabiki kununua tiketi mapema sio kusubiri hadi siku ya mchezo.

Kamwe aliwataka mashabiki kunua tiketi kwa wingi ili kujaza uwanja katika mchezo huo na kuwapa wachezaji nguvu ya kuipambania timu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live