Klabu ya Yanga imebakiza alama 10 pekee ili iweze kuutetea ubingwa wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara kwa mara nyingine tena kati ya alama 18 ambazo klabu hiyo imebakiza.
Kwa hesabu za kawaida Yanga inahitaji kushinda michezo mitatu [3] walau na sare moja (1), kati ya michezo sita (6) ambayo klabu hiyo imebakiza hadi hivi sasa.
Matokeo hayo yatategemea michezo ijao ya wapinzani wao wanaowafuata Azam (Mechi 24, 54 pts), Simba (Mechi 22, 47 pts)
Michezo ijayo ya Yanga
- vs Mashujaa (A)
- vs Kagera (H)
- vs Mtibwa Sugar (A)
- vs Dodoma Jiji (A)
- vs Tabora United (H)
- vs TZ Prison (H)
Je, Yanga itaweza kuangazia ubingwa wake Jijini Dodoma ?