Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kutambulisha jezi za msimu mpya leo

Yanga Sc Mabadiliko 2 @binzubeiry Mkurugenzi wa uwekezaji Injinia Hersi Said (aliesimama) na Viongozi wa Yanga

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Dar es Salaam Young Africans leo hii wanaenda kutambulisha jezi zao mpya kwa msimu mpya wa 2021/2022.

Yanga wanaenda kutambulisha jezi watakazotumia nyumbani msimu ujao, ugenini pamoja na jezi ya ziada.

Tukio hilo linatarajiwa kufanyika leo Agosti 25, katika ukumbi wa Mlimani City na pia Mashabiki watapata nafasi ya kununua jezi huku wakielekea katika kilele cha wiki ya mwananchi Jumapili ya wiki hii.

Yanga katika shughuli hiyo itaambatana na Afisa Habari mpya wa klabu hiyo, Haji Manara katika kunogesha tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live