Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kutambulisha benchi zima la ufundi

Gamondi Yanga Yanga kutambulisha benchi zima la ufundi

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya yanga, Ally Kamwe amesema kuwa klabu hiyo bado haijamaliza kutangaza wachezaji na viongozi ambao wataachwa na klabu hiyo kuelekea msimu mpya.

Kamwe amesemwa hayo leo Jumatatu, Julai 3, 2023 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar akielezea mambo mbalimbali kuhusu klabu hiyo kuelekea msimu mpya.

"Tumeshatambulisha kocha mkuu, Miguel Gamondi kutoka Argentina, wiki hii ataingia nchini. Watu wanauliza wasaidizi wake watakuwa kina nani iwapo waliopo tutawaacha au wataendelea. Niwaambie kuwa siku Kocha Mkuu akifika nchini ndiyo siku ambayo tutatambulisha benchi letu zima la ufundi.

"Kuanzia Kocha Msaidizi, Physio, Fitness Coach, daktari, meneja, video analyst, kifupi ni safu nzima ya benchi la ufundi. Kwa hiyo mtapata majibu palepale nani ameondoka nani amebaki," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: