Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kushusha vifaa vipya

Ally Kamwe Awajibu Mashabiki Young Africans.png Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema baada ya kukamilisha kuboresha maslahi ya mastaa wao wanaowahitaji kabla ya dirisha dogo kufungwa watashusha wachezaji wawili wapya.

Kamwe amesema wanachokifanya sasa ni kuboresha kikosi chao kwa kuongeza mikataba mastaa wote ambao benchi la ufundi limependekeza kuendelea kuwa nao wakianza na kipa Djigui Diarra na Khalid Aucho.

“Bado tunaendelea kumalizana na wengine hivi karibuni tutatangaza mwingine ambaye ameboreshewa mkataba na baada ya kukamilisha hao kazi itaanza kwa mastaa wengine wakubwa wanaojiunga na timu yetu,” anasema na kuongeza;

“Timu kubwa inabakiza wachezaji wake muhimu kwa kuboresha maslahi yao na kuendelea kuwa nao kwenye timu hicho kimefanyika na kitaendelea kufanyika lengo ni kuhakikisha tunakuwa bora,”.

Kamwe anasema kabla ya Januari 15 watafanya kitu kikubwa kwenye nchi hii kwa kumtambulisha mchezaji mkubwa ambaye amewahi kucheza soka kwenye timu kubwa.

Chanzo: Mwanaspoti