Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kusaka makali kwa JKU

Hersi X Gamondi Usajili Yanga kusaka makali kwa JKU

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi aliagiza uongozi wa timu hiyo kumtafutia michezo angalau miwili ya kirafiki kwa ajili ya kukipima kikosi chake, na sasa timu hiyo itaanza kujipima na JKU ya Zanzibar kabla ya kurejea katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo wa kwanza wa kirafiki utachezwa Jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa Yanga wamelazimika kusaka mechi za kirafiki mapema baada ya Gamondi kuwaambia wafanye kila linalowezekana kupata mechi za haraka kabla ya kurejea kwa Ligi Kuu.

Hata hivyo, kutoka ndani ya klabu hizo zinasema wamekubaliana kuhusu kucheza mechi hiyo ya kirafiki na JKU na wapo kwenye mchakato wa kusaka timu nyingine ya pili kukamilisha hitaji la kocha Gamondi.

Akizungumza na gazeti hili, Gamondi amesema kuna kila sababu ya timu yake kupata mechi za kirafiki, ikiwezekana pia na mchezo mmoja wa kimataifa wa kirafiki wakati huu wa mapumziko ili kujua ubora wa kikosi chake na kuona muunganiko alioutengeneza.

“Tumerejea mapema kwenye mazoezi kuweza kujipanga kwa muda huu ambao upo kwa sasa, unajua tuna wachezaji wapya ambao wamesajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo la usajili, tupo nao kwenye mazoezi hivyo ni vizuri kupata michezo ya kirafiki kuangalia kikosi chetu," amesema Gamondi na kuongeza,

"Tunalenga kuboresha timu yetu tukiwa na malengo ya kufanya vizuri kimataifa, michezo hii ya kirafiki baada ya kuongeza wachezaji itanipa picha ya nini napaswan kuongeza au kuboresha," amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: