Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kusafiri na Mashabiki mechi ya Rwanda

Basi La Yanga.jpeg Yanga kusafiri na Mashabiki mechi ya Rwanda

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga inaandaa mpango wa kusafiri na Mashabiki wake kuelekea Rwanda katika mchezo wa mtoano kuwania kufuzu kwa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga watacheza na Al Merrikh Septemba 16, nchini Rwanda na tayari Afisa Habari Ally Kamwe ameshatoa utaratibu;

"Tutakuwa na mabasi rasmi ambao Uongozi wa Young Africans umeendaa. Kila ambaye anahitaji kwenda atahitajika kutoa kiasi cha tsh. 150,000 ikiwa ni nauli ya kwenda na kurudi. Utaratibu wa kula kunywa na kulala kila mtu atajitegemea mwenyewe. Hata hivyo kila mtu atapaswa kuwa na hati ya kusafiria.

Tumepokea jumbe mbalimbali kutoka Rwanda wakitusubiria kwa hamu kubwa. Rwanda nzima inayo kiu kubwa ya kutupokea. Misafara yote itaondoka siku moja. Kwa wale wanaotumia basi wataondoka hapa tarehe 14.09.2023 saa 11 alfajiri, na kwenda kulala Kahama kabla ya kuelekea Rwanda. Kurudi itakuwa tarehe 17 au tunaweza kuongeza siku"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: