Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kurudishwa Tabora tena

Uwanja Wa Ali Hassan Mwinyi 80387 Yanga kurudishwa Tabora tena

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Nchini (TFF) limeufungulia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliopo Mkoani Tabora kuendelea kutumika katika michezo ya NBC Premier League baada ya kufanyiwa marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni za sheria za mpira wa miguu.

Dimba hili hutumiwa kama uwanja wa nyumbani wa Timu ya Tabora United inayocheza ligi kuu msimu huu.



Huenda mchezo wa Yanga dhidi ya Tabora ukarejeshwa tena katika Dimba la Ali Hassan Mwinyi baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), hapo awali kufanya mabadiliko ya uwanja wa mchezo na kuupeleka Jamhuri Dodoma.

Mchezo huo namba 110, ambao timu Yanga SC itakuwa ugenini, sasa ulipangwa kuchezwa Desemba 23, 2023, saa 1:00 Usiku kwenye Uwanja wa Jamhuri uliopo Dodoma huku sababu za mabadilko hayo ni Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kufungiwa na Kamati ya Leseni za Klabu ya TFF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live