Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kupiga mechi tano Februari

Simba Vs Yanga Nov 5 Maxi.jpeg Yanga kupiga mechi tano Februari

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imetoa ratiba ya muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2023-2024.

Katika ratiba hiyo, zitaanza mechi za viporo ambapo timu ya Young Africans SC itacheza mechi tatu.

Ratiba hiyo inaonesha kwamba, ndani ya mwezi Februari pekee, Young Africans SC itacheza mechi tano, mbili ikiwa mwenyeji na tatu ugenini.

Mechi tano za kwanza kwa mujibu wa ratiba hiyo ipo hivi;

Februari 2, 2024; Kagera Sugar vs Yanga kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Februari 5, 2024 ni Yanga vs Dodoma Jiji, hii itachezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Februari 8, 2024, Yanga vs Mashujaa, itachezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Februari 11, 2024 ni Tanzania Prisons vs Yanga, itachezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Kisha Februari 17, 2024 ni KMC vs Yanga, hii haijapangiwa uwanja mpaka sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live