Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kupeleka ujumbe mzito CAF msimu huu

Yanga Kamweeeee Ally Kamwe na mashabiki wa Yanga.

Mon, 19 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC, Ally Kamwe, amesema msimu huu kuna ujumbe wanaupeleka kwenye michuano ya kimataifa iliyoanza wikiendi iliyopita.

Young Africans wanashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo hatua ya awali wanacheza dhidi ya Vital’O ya Burundi huku wakishinda mechi ya kwanza magoli 4-0. Marudiano yatakuwa Jumamosi ya wiki hii.

Baada ya ushindi mnono wikiendi iliyopita, Kamwe amesema hizo ni salamu kwa washiriki wote wa michuano hiyo kwa msimu huu.

“Kupitia mashindano ya CAF, hatua hizi za awali, kuna ujumbe tunataka kuupeleka kwa wale ambao wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa AFRIKA. Tutatuma ujumbe ndani ya uwanja na nje ya Uwanja. Nje ya uwanja tulituma ujumbe msimu uliopita kwa kujaza uwanja wa ugenini,” alisema Kamwe.

Kuhusu kauli mbiu za mchezo kama ilivyokuwa msimu uliopita, Kamwe amesema utaratibu huo utaendelea kwa mtindo tofauti kutokana na ubunifu mkubwa ulionao Idara ya Habari ya Young Africans SC.

“Kauli mbiu za Mchezo zitaendelea kuwepo kama kawaida. Tulichoondoa ni kuzipa mechi majina ya wachezaji. Lakini niwaeleze tu kuwa idara yetu ya habari ina watu wenye ubunifu wa kila namna. Tutaendelea kuja na aina tofauti tofuati ya mbinu za kutangaza michezo yetu ya kimataifa. Hatutaki kuwa na ubunifu unaojirudia rudia,” alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live